Wazazi wanahimizwa kuhakikisha watoto walio chini ya miaka mitano wanapata chanjo zote za kawaida na za nyongeza ili kuwalinda kutokana na magonjwa katika utoto na hadi utu uzima. Daktari wa watoto Alan Toh anasema watoto barani Afrika wako katika hatari zaidi ya kupata magonjwa mbalimbali, na kufanya chanjo kuwa muhimu katika kuongeza kinga yao. Anaongeza kuwa chanjo ni salama na zinapaswa kutolewa kama ilivyopendekezwa.

ALAN TOH - VACCINES