Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, ameikosoa serikali kwa ushuru mkubwa, akiitangaza Kenya kuwa moja ya mataifa yanayotozwa ushuru kupita kiasi duniani. Akizungumza mjini Mombasa, Kalonzo alisema kwamba ushuru unaoingiliana kutoka kwa serikali kuu na kaunti unawalemea raia wa kawaida, akibaini kuwa mamilioni ya Wakenya wametumbukia kwenye umaskini kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

KALONZO MUSYOKA - TAXATION