Chama cha Soka cha Afrika Kusini kimethibitisha kwamba Pitso Mosimane anakaribia kuteuliwa kuwa kocha wao mkuu mpya, huku masharti yakisubiriwa. Chama hicho kinasema uteuzi wa Mosimane uliruhusiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Kitaifa Jumamosi jijini Johannesburg. Anachukua nafasi ya Hugo Broos, ambaye aliondoka kama kocha mkuu wa Bafana Bafana mnamo Julai tarehe 31 baada ya zaidi ya miaka mitano kuiongoza. Mbelgiji huyo aliiongoza Afrika Kusini hadi nafasi ya tatu katika AFCON ya mwaka 2024, na raundi ya 32 katika Kombe la Dunia mwaka huu.
Beki wa kati wa Tottenham Micky van de Ven ametia saini mkataba mpya wa kuongeza muda wake wa kukaa North London hadi mwaka 2031, huku chaguo likiendelea hadi mwaka 2032. Raia huyo wa Ducth ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa unaisha 2028-29 anajiunga na mshindi wa Kombe la Dunia wa Uhispania Pedro Porro na kipa wa Czech Antonín Kinsky katika kutia saini mkataba mpya msimu huu wa joto. Usajili huo unakuja miezi michache tu baada ya Spurs kuepuka kushushwa daraja kutoka Ligi ya Primia chini ya kocha mpya Roberto De Zerbi kwa ushindi wa siku ya mwisho dhidi ya Everton.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.