Rais William Ruto amewahimiza viongozi wa kisiasa kuweka kando tofauti zao na kuzingatia kutekeleza ilani ya serikali. Akihutubia viongozi wakati wa mkutano mkuu wa serikali unaoendelea huko Naivasha, Rais alisema Kenya inaweza kufikia uwezo wake kamili ikiwa viongozi wake watabaki kuwa wamoja. Alisema uamuzi wake wa kuwasiliana na marehemu RailaOdinga baada ya uchaguzi wa 2022 ulitokana na hitaji la kuunganisha nchi.

WILLIAM RUTO - LEADERS