Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amelitaka eneo la Mlima Kenya kukataa siasa za mgawanyiko na kubaki na umoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao. Waiguru anasema eneo hilo limenufaika kihistoria kutokana na maendeleo kwa kufanya kazi na serikali badala ya kubaki katika upinzani. Aliwataka viongozi na wakaazi kuweka kando tofauti za kisiasa na kufuata mbinu ya umoja ambayo italinda maslahi na faida za maendeleo ya eneo hilo.
ANNE WAIGURU – UMOJA