Wahudumu wa boda boda wamehimizwa kujitenga na wanasiasa wanaotaka kuwatumia vibaya ili kuchochea machafuko na vurugu wakati wa kampeni. Akizungumza katika kikao cha mafunzo ya usalama barabarani huko Kapsabet, Kaunti ya Nandi, Mwenyekiti wa Kitaifa wa Chama cha Usalama wa Boda Boda cha Kenya Kevin Mubadi pia aliwataka waendesha boda boda kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya usalama ili kutambua na kuondoa wahalifu ndani ya sekta ya boda boda.
KEVIN MUBADI - TUMIKA