Viongozi wa kisiasa kutoka Mt Elgon wametaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu mauaji ya MCA wa Chesikaki Nathan Wasama, ambaye alipigwa risasi na washambuliaji wasiojulikana Alhamisi usiku. Viongozi hao, wakiwemo wagombea wa Uchaguzi Mkuu wa 2027, waliiomba serikali kuwatambua, kuwakamata na kuwashtaki haraka wale waliohusika. Pia walimwomba Waziri Kipchumba Murkomen kuingilia kati na kuimarisha usalama ili kuwalinda wakaazi na viongozi wa kisiasa.
KIBOI KOSUM - SECURITY