Mashabiki wa Manchester United waliwashinda mashabiki wa Arsenal kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Nyayo jana, na kukamilisha ushindi mara mbili baada ya ushindi wa 3-2 katika mechi ya kwanza kwa hisani ya Sportpesa. Mchekeshaji Yasin na Jian waliweka kikosi cha Uinted mbele mapema kabla, Machwani na Telvin Paul kujibu kwa Arsenal katika kipindi cha pili. Eric Omondi ambaye alikuwa nahodha wa waundaji wa maudhui wa United alifunga penalti ya ushindi na kuwashinda mashabiki wa Arsenal waliofunzwa na Ghost Mulee. Mchekeshaji Tumbili aliomba kampuni kudhamini mashabiki wa KPL ili kukuza ligi hiyo ya ndani.

 


Nahodha wa zamani wa Sofapaka Clifton Miheso kwa sasa anafanya mazoezi na Tusker FC baada ya kuachana na Batoto ba Mungu. Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa Brewers watampatia winga huyo mwenye uzoefu mkataba. Miheso ambaye aliacha Sofapaka baada ya kushushwa daraja msimu uliopita alikuwa amehusishwa na Bandari, lakini uhamisho huo haukufanikiwa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya ambaye alikuwa katika kipindi chake cha pili huko Sofapaka, hapo awali alichezea Thika United, AFC Leopards na Gor Mahia.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.