Mabingwa Nigeria walitolewa nje ya mashindano ya WAFCON katika robo fainali baada ya kufungwa 1-0 na Cameroon mjini Rabat jana usiku. Bao la dakika ya 20 la Miriam Nyadjou liliifanya Indomitable Lionesses kumaliza safari ya Super Falcon. Wakati huo huo, Malawi ilijitahidi kutoka nyuma na kuishinda Ghana 2-1 kwa bao la ushindi la dakika za lala salama kutoka kwa Rose Kadzere. Chantelle Boye aliiweka Ghana mbele katika dakika ya 7, lakini Temwa Chawinga alisawazisha dakika tano baadaye. Cameroon itapambana na wenyeji Morocco katika nusu fainali, huku Malawi ikikabiliana na Algeria Jumatano.

 

Rais wa LaLiga, Javier Tebas, anadai Gianni Infantino anaharibu kiini cha mpira wa miguu na anaamini wakati wake kama rais wa FIFA umefika mwisho. Infantino amekabiliwa na ukosoaji kufuatia mpango wake ulioshindwa wa kutafuta uwekezaji binafsi katika kampuni ambayo ingeendesha mashindano ya FIFA na kuuza hisa katika Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi. Licha ya FIFA kusimamisha mipango hiyo na kuomba msamaha kwa vyama vya kitaifa wiki iliyopita, UEFA na Chama cha Soka wamemtaka Infantino ajiuzulu.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.