Serikali imehimizwa kuwekeza katika sekta zinazochipukia kama vile uchumi wa kidijitali na tasnia ya ubunifu kama juhudi za kushughulikia ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana. Akizungumza wakati wa sherehe ya kwanza ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Zetech huko Mang’u, Mkurugenzi wa Masuala ya Biashara na Masoko wa Zetech John Mwai alisema serikali inapaswa kuunda miundombinu ili kusaidia ujuzi mpya na kurahisisha vijana kupata ufadhili. Aliwasihi vijana kuangazia zaidi ya kazi za kitamaduni na kukumbatia fursa ambapo wanaweza pia kuunda ajira kwa wengine.
JOHN MWAI – SKILLS