Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Oburu Oginga wanaongoza viongozi wao katika mkutano wa mkakati wa kisiasa unaolenga kukabiliana na mashambulizi yanayoongezeka ya upinzani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao. Warsha hiyo ya siku mbili ya viongozi waliochaguliwa wanaoshirikiana na serikali pana inaanza leo mjini Naivasha na kuwakutanisha wabunge kutoka Kenya Kwanza na ODM.