Jamii za wafugaji katika kaunti za Isiolo, Laikipia, Samburu na Meru zitanufaika na miradi minne ya maji inayofadhiliwa kupitia mapato kutoka kwa mbio za kwanza za barabarani za Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Ukame NDMA kwa ajili ya amani na ustahimilivu zilizofanyika katika Archers Post, Kaunti ya Samburu. Hafla hiyo ililenga kukusanya zaidi ya Sh milioni 130 ili kuboresha upatikanaji wa maji na kusaidia kupunguza migogoro inayotokana na rasilimali miongoni mwa jamii katika eneo hilo kwa ujumla, na kuboresha maisha. Huyu hapa Mkurugenzi Mtendaji wa NDMA Hassan Adan.

HASSAN ADAN - CHALLENGE