Mwanamume mwenye umri wa miaka 24 anadaiwa kuuawa kwa kudungwa kisu wakati wa malumbano na kakake katika eneo la Shivala, kaunti ya Kakamega. Polisi walisema tukio hilo lilimhusisha Ibhrahim Lutta, 24, ambaye inadaiwa alishambuliwa na kakake mwenye umri wa miaka 32. Polisi walitembelea eneo la tukio na kukuta mwili wa Ibhrahim ukiwa umelala chali, ukiwa na jeraha la kudungwa kisu kifuani.  Mshukiwa alikamatwa na umma na kukabidhiwa kwa polisi.