Shirika la Umoja wa Maimamu huko Nakuru limeonya kwamba kauli za kisiasa zinazolenga kukandamiza sauti za upinzani zinadhoofisha demokrasia. Wakizungumza huko Nakuru, viongozi wa kidini walisema hakuna taifa linaloweza kustawi wakati upinzani unanyamazishwa. Waliwasihi viongozi kukuza amani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao kwa kuepuka kuchafua makabila na kukumbatia mazungumzo, umoja, na uvumilivu.
ATHUMAN MASOOD - TUME