Ujenzi wa kitengo cha uzazi chenye thamani ya Sh40 milioni umeanza katika Zahanati ya Nyaribo katika Kaunti ya Nyeri, ukiashiria hatua kubwa kuelekea kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za afya ya mama na mtoto. Katibu wa Huduma za matibabu OumaOluga alisema mradi huo utapunguza umbali ambao wakaazi husafiri kutafuta huduma, kuboresha utoaji wa huduma, na kuunga mkono lengo la serikali la kufikia Bima ya Afya kwa Wote.