Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameihimiza serikali kuharakisha na kukamilisha Bwawa la Koru-Soin katika Kaunti ya Kisumu ili kutoa maji kwa ajili ya unyunyuzaji na kushughulikia changamoto zinazohusiana na maji wakaazi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa mazishi ya Elvis Otieno, mbunge huyo alisema kwamba bwawa hilo litasaidia kupunguza mafuriko ambayo yamekuwa yakiwakumba wakaazi wa Awasi na maeneo mengine ya karibu.
BABU OWINO - DAM