Idara ya Makaazi ya serikali inasema ripoti kwamba Wakenya walitoa Sh bilioni 2.56 kutoka kwa mpango wa akiba wa Boma Yangu zinapotosha. Katibu wa Makaazi Charles Hinga anasema karibu asilimia 69 ya kiasi hicho hakikuwa marejesho ya pesa taslimu bali akiba iliyotumika kama amana kununua nyumba za bei nafuu. Idara hiyo inaongeza kuwa uondoaji halisi wa pesa taslimu ni Sh milioni 803, huku jumla ya akiba kwenye mfumo huo ikiwa imeongezeka mara mbili hadi Sh bilioni 5.47, huku watumiaji waliosajiliwa wakiongezeka hadi milioni 1.26.
CHARLES HINGA – WITHDRAWALS