Shirika la kuetetea haki za binadamu MUHURI limelaani wito wa Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua kwa watalii na wawekezaji kuepuka Kenya, likisema matamshi kama hayo yanatishia maisha na uchumi wa nchi. Likiongozwa na Francis Auma, shirika hilo lilisema ingawa vurugu za kisiasa na uhuni lazima zishughulikiwe, kukataza usafiri na uwekezaji huwaadhibu Wakenya wa kawaida tu. Wamentaka Gachagua kuomba msamaha na kuitaka serikali  kuchukua hatua madhubuti kukomesha vurugu za kisiasa.

FRANCIS AUMA – GACHAGUA