Wahudumu wa afya wanatarajiwa kuandamana jijini Nairobi leo, wakidai ajira ya kudumu na ya kustaafu kwa wafanyakazi wa UHC. Maafisa wa kliniki, wataalamu wa lishe na mafundi wa maabara wanapinga kushindwa kwa kaunti kutoa barua za uteuzi licha ya Wizara ya Afya kutoa fedha kwa ajili ya mchakato huo na kukubali kuzitoa kama fedha za usawa. Wahudumu hao walianza mgomo wao wa kitaifa Jumatatu.
PETERSON WACHIRA – PROTESTS