Wadau wa sekta ya utalii wanaonya kwamba matamshi mabaya ya kisiasa yanaweza kuathiri ajira na biashara zinazotegemea wageni. Shirikisho la Utalii la Nchini na vyama vya utalii vya kikanda vinasema safari zilizofutwa na uwekezaji ulioahirishwa huathiri moja kwa moja wafanyakazi wa hoteli, wasafirishaji watalii, waendeshaji usafiri, mafundi na wakulima. Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo amejiunga na wale wanaomlaani Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua kwa matamshi yake kwamba watalii waepuke kuja Kenya.


STEWART MADZAYO – REMARKS