Tume ya EACC imechukua hatua ya kurejesha ekari 7.6 za ardhi ya Huduma ya Magereza ya Kenya katika eneo la Milimani huko Kisumu, ambalo inasema lilibadilishwa kinyume cha sheria na isivyo halali kuwa mali ya kibinafsi. Ardhi inayozozaniwa ina thamani ya takriban Sh milioni 790, ukiondoa ujenzi. Mkurugenzi Mtendaji wa EACC Abdi Mohamud anasema thamani hiyo inaongezeka hadi takriban Sh bilioni 4.3 wakati ujenzi wa mali hiyo unapojumuishwa.

ABDI MOHAMUD – LAND