Mshukiwa wa mauaji ambaye alikiri kumuua kaka yake mkubwa ameamriwa kufanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi kabla ya kesi yake kuendelea katika Mahakama Kuu ya Eldoret. Albert Kiprop, 34, alifika mbele ya Mahakama Kuu ya Eldoret jana ambapo alikiri shtaka la mauaji linalohusiana na kifo cha kaka yake Daniel Ngetich. Kiprop aliishtua mahakama alipokiri waziwazi kumuua Ngetich, 54, kwa kutumia kitu chenye ncha kali wakati wa tukio lililoripotiwa kutokea katika kijiji cha Chelelmetio katika Kaunti Ndogo ya Moiben, Kaunti ya Uasin Gishu mwezi uliopita.