NAIROBI, KENYA, Julai 27, 2025 — Mbunge wa Suba North, Mille Odhiambo, ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kuonekana kwenye video akiangusha densi jukwaani katika kongamano la kuwawezesha wanawake lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Video hiyo iliposambaa, baadhi ya wananchi na wanaharakati wa mitandaoni walimshutumu kwa kile walichokitaja kuwa “tabia isiyo ya heshima kwa kiongozi wa umma.”

Katika kujibu, Mille hakusita kuonesha msimamo wake kwa lugha ya kejeli na utani.

Millie Odhiambo na Farouk Kibet

“Ninasikia watu wengine wamekuwa PSD kwa sababu nilicheza kwenye kongamano la kuwawezesha wanawake baada ya kusukumwa kidogo na Farouk Kibet,” alisema kupitia video aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii.

Mbunge huyo anayefahamika kwa ujasiri wa kutoa kauli zisizoficha, aliendelea kusisitiza kuwa haoni kosa lolote katika kuonyesha furaha yake hadharani.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Nitacheza kokote na wakati wowote, iwe nimesukumwa au la. Kucheza kumenijenga kimaumbile na sitakoma hata kaburini, omera. Ukiudhika, nenda kwa polisi,” aliongeza kwa msisitizo.

Kauli hizo ziliwavutia wafuasi wake wengi waliomuunga mkono kwa kusema kuwa yeye ni mtu wa watu na asiyejificha nyuma ya vyeo vya kisiasa. Lakini wengine waliona ni utovu wa nidhamu na mfano usiofaa kwa viongozi.

Millie Odhiambo

Katika kujitetea zaidi, Mille alisema:

“Hii nchi inahitaji viongozi walio hai, si wa plastiki. Msiwe mnataka viongozi wanaocheka kwa script. Mimi siwezi kuvaa sura ya huzuni kila siku eti kwa sababu mimi ni mbunge.”

Aliwashauri wakosoaji wake kuelekeza nguvu zao kwa masuala muhimu kama vile ufisadi na ukosefu wa huduma bora kwa wananchi, badala ya kujadili dansi ya sekunde 30.

“Wanawake wakicheka hadharani, mnaita uhuni. Wanaume wakicheka, mnaita charisma. Huo ni unafiki wa kijinsia,” alitoa changamoto.

Millie Odhiambo