
Kiongozi wa ODM Raila Odinga ameungana na nchi kuomboleza kifo cha mlinzi na msaidizi wake wa muda mrefu, George Odwuor, aliyeaga Jumatano.
Oduor alilazwa katika hospitali ya Nairobi West kwa wiki mbili kabla ya kuaga Jumatano jioni.
Alikuwa mshirika wa karibu wa Raila kwa miaka mingi na alikuwa mtu anayefahamika katika hafla na shughuli za Raila.
"Ni kwa mshtuko mkubwa na huzuni kwamba ninatangaza kuaga kwa msaidizi wangu wa kibinafsi na mlinzi George Oduor jioni ya leo Nairobi baada ya kuugua kwa muda mfupi," Raila alisema katika ujumbe.
"George amekuwa sehemu ya Jaramogi na familia yangu tangu mwishoni mwa miaka ya 80. Tumesimama, tumeanguka na kuinuka pamoja. Amekuwa macho, mtulivu, anayejiamini, na msaidizi wa kitaalamu aliyejitolea kwa ajili ya wajibu na mwamba wa kutegemewa upande wangu miaka hii yote kupitia vipindi vya misukosuko. Nitamkosa George, na ninasikitika kwa marafiki wengi ambao tayari wamemkosa, "aliongeza.
"Kwa mkewe, Carol George, familia nzima, wafanyakazi wenzake, na marafiki, ninawapa Mama Ida na familia nzima ya Jaramogi rambirambi kwa msiba huu mbaya," Raila alimalizia.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!