WAZIRI wa usalama wa ndani, Kipchumba Murkomen amewasuta wanaandishi wa habari wanaochapisha simulizi alizozitaja kuwa za kufurahisha lakini zisizo na ukweli kuhusu hali ya usalama nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Kitaifa wa Washirika wa Maendeleo ya Huduma ya Polisi katika Shule ya Serikali ya Kenya Jumatano, Murkomen alisema kwamba baadhi ya waandishi wa habari wanatunga simulizi za kuvutia zisozo na mashiko kuhusu hali ya usalama wakiwa katika ofisi zao jijini Nairobi.
Waziri huyo alidai kwamba yuko tayari kufadhili ziara ya siku 5 kwa wanahabari kutoka Nairobi kuwapeleka katika mji wa El Wak kaunti ya Mandera ili kuona jinsi polisi wanafanya oparesheni ya amani.
“Najua ni rahisi sana kwa watu kuketi nyuma ya kompyuta zao na kuandika hadithi kuhusu maafisa wetu wa polisi. Ninaona mara nyingi sana. Natamani kwamba tungeweza kuwabeba baadhi ya wahariri hawa, waandishi wa habari, na wanablogu-sio kwa siku nzima, lakini kwa nusu siku-hadi maeneo ya kazi kama Elwak,” Murkomen alisisitiza.
"Ninataka kuwaomba wanahabari wote ambao wanaandika habari nzuri sana kutuhusu Nairobi kwamba nitawapa usafiri bila malipo na kuwasafirisha kwa ndege idadi kubwa ya wanahabari hadi Elwak. Nataka walale huko kwa wiki moja."
Kulingana na Murkomen, vyombo vya habari vimekuwa vikichapisha taarifa kuhusu wizara yake zisizo sahihi na kulifanya suala la usalama kuonekana kama mzaha na anataka kuwapeleka ‘ground’ wahisi uzito wa suala la usalama.
Waziri huyo amekuwa akishambuliwa katika siku za hivi karibuni haswa kutokana na ongezeko la visa vya uhalifu wa wizi wa mifugo na majangili ya kusmabulia watu katika Maeneo mbalimbali humu nchini.
Wa hivi punde kumkashifu ni mwezake serikalini, seneta wa Nandi Samson Cherargei ambaye amesisitiza kwamba Murkomen hafai kushikilia wizara ya usalama wa ndani.
“Nilichoona miaka miwili iliyopita kuhusu CS Murkoman ni INCOMPETENCE sasa kinaweza kuonekana !! angalau uzembe katika wizara ya barabara ulimaanisha kuwa inaweza kurekebishwa baadaye LAKINI uzembe katika usalama wa ndani maana yake maisha yanapotea ambayo hayawezi kurejeshwa!” alisema Cherargei.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!