
PROF. Julius Bitok na Dkt. Belio Kipsang wamebadilishana majukumu kama makatibu wa wizara zao katika mabadiliko mapya ya rais William Ruto.
Bitok amehamia Idara ya Elimu ya Msingi chini ya wizara ya elimu huku Kipsang akiwa PS wa Idara ya Uhamiaji na Huduma kwa Raia chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa.
Makatibu wengine ambao walihamishwa katika wizara zao ni pamoja na Elijah Mwangi ambaye sasa Naibu Katibu Mkuu mpya wa Idara za Serikali za Michezo katika Wizara ya Masuala ya Vijana na Michezo.
Mwangi alikuwa PS, Idara ya Serikali ya Madini katika Wizara ya Madini, Uchumi wa Bluu na Masuala ya Bahari.
Teresiah Mbaika ameteuliwa kuwa katibu wa Idara ya Serikali ya Usafiri wa Anga na Maendeleo ya Anga katika Wizara ya Barabara na Uchukuzi.
Mbaika amekuwa akihudumu kama katibu katika Idara ugatuzi chini ya Ofisi ya Naibu Rais.
Ismael Madey amehamishwa kutoka Idara ya Serikali ya Masuala ya Vijana hadi Idara ya Serikali kwa ajili ya Mipango Maalum katika Wizara ya Utumishi wa Umma, Maendeleo ya Rasilimali ya Watu na Mipango Maalum.
Harry Kimtai amepewa kazi nyingine katika Idara ya wizara ya Madini na uchumi wa baharini. Kimtai amekuwa akifanya kazi kama katibu katika Idara ya Huduma za Matibabu chini ya Wizara ya Afya.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!