Kalonzo Musyoka amtaka Ruto kuwapa mama mboga kandarasi ya kupika na kusambaza chapati shuleni//FACEBOOK


KIONGOZI wa chama cha WIPER, Kalonzo Musyoka amempa rais William Ruto changamoto ya kuwainua watu wa maisha ya chini kama kina mama mboga kwa kuwapa kandarasi ya kupika chapati na kuzisambaza kwa shule za Nairoi.


Akizungumza Jumamosi, Kalonzo alisema kwamba rais Ruto hakufurahia kutangaza kwamba anataka kununua mashine ya kupika chapati kwa ajili ya wanafunzi Nairobi wakati kuna watu wengi wenye uwezi wa kupika chapati hizo.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alimtaka Ruto kama kweli ana nia ya kuwakimu kiuchumi mama mboga kama alivyowaahidi wakati wa kampeni, basi awape zabuni hiyo ya kupika chapati badala ya kuipa kazi hiyo mashine.


"Kimsingi ni wazo zuri kula chapati, lakini kwa nini usimpe Mama Mboga huko Kangemi, Utawala, Mathare, kandarasi ya kutengeneza chapati hizo na kuzisambaza kwa Shule ya Msingi ya Toi na sehemu zingine?" alimwambia.


Kalonzo pia alikejeli matamshi ya hivi majuzi ya Rais kuhusu lakabu zake nyingi, akirejelea pendekezo la Ruto kwamba orodha yake inayoongezeka ya majina inaweza kuendana na miaka yake ya uongozi.


“Na anasema amepewa majina sita na anasubiri yawe kumi ili apate miaka yake kumi. Nadhani afya ya akili ni hali hapa - kwamba anafikiri kwamba kumpa majina kumi ambayo yote yamefafanuliwa vizuri hutafsiri kuwa miaka kumi. Uongo,” Musyoka alisema.


Mnamo Jumanne, Machi 11, 2025, Rais Ruto aliahidi kununua mashine ya kutengeneza chapati ili kuimarisha mpango wa kulisha shule wa Dishi na County wa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja.


Ahadi hiyo ilitolewa baada ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya St. Teresa huko Mathare kueleza hamu yao ya kuwa na chapati kwenye menyu kufuatia uchunguzi wa Sakaja kuhusu upendeleo wa chakula.


Sakaja hata hivyo, aliibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuandaa chapati kwa zaidi ya wanafunzi 300,000 na akaomba mashine ya kushughulikia kazi hiyo.


Hatua ya kuahidi kununua mashine ya kupika chapati milioni moja kila siku kwa ajili ya kupiga jeki mpango wa Dishi na County imezua mchecheto mitandaoni, wengi wakionekana kumkashifu rais kwa kile wanadai anapatia kipaumbele masuala ambayo si ya kutatua masuala nyeti yanayowakumba wananchi walio wengi.