
MBUNGE wa Embakasi Mashariki, Babu Owino amekuwa wa hivi punde kutoa wito wa kipekee kwa rais William Ruto kuwasiliana na serikali ya Vietnam ili kuzuia kunyongwa kwa Mkenya Margaret Nduta.
Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Owino alimrai rais Ruto kuwasiliana na mwenzake wa Vietnam ili kuzuia kunyongwa kwa Mkenya huyo kunakotarajia kufanyika usiku wa Jumapili, Machi 16.
Margaret Nduta anasubiriwa hukumu yake ya kunyongwa na serikali ya Vietnam baada ya kukutwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege.
Akimtetea, Owino alidai kwamba Nduta hakutekeleza uhalifu wowote, bali yeye ni mwathirika wa matukio aliyejipata katika sehemu mbaya wakati mbaya.
“Napenda kuchukua fursa hii kumuomba na kumrai Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto, amsaidie bibi huyu aitwaye Margaret Nduta anayedaiwa kunyongwa kesho huko Vietnam, huyu bibi hakufanya kosa lolote, alikuwa mahali pasipostahili kwa wakati mbaya, alitumika kusafirisha dawa za kulevya,” alisema Babu.
Alipendekeza zaidi kwamba ikiwa mazungumzo yatahitajika, Kenya inaweza hata kubadilishana afisa wa serikali fisadi kwa uhuru wake.
"Hatufai kumpoteza Mkenya, Bw. Rais. Unahitaji kuchukua hatua kwa haraka. Msaidie Margaret Nduta. Asinyongwe. Ninajua kwamba unaweza kuchukua simu yako na kuipigia serikali ya Vietnam. Sisi kama Wakenya tunahitaji kuungana nyuma ya bibi huyu. Hata ikimaanisha kubadilishana naye mmoja wa Mawaziri fisadi, tufanye lolote tuwezalo kuokoa maisha ya Margaret."
Huku muda ukizidi kuyoyoma, sasa inasubiriwa kuonekana ni hatua gani ambayo itachukuliwa kuhakikisha hukumu hiyo ya Nduta kunyongwa inahairishwa ili kutoa muda wa majadiliano zaidi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!