Dola za Kimarekani na sarafu za Kenya

MWANAMKE mmoja anayeshukiwa kutoroka na bidhaa za thamani kutoka kwa mwajiri wake hatimaye ametiwa mbaroni na makachero wa idara ya upelelezi, DCI mtaani Kawangware, Nairobi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa na DCI kwenye ukurasa wao wa X, mwanamke huyo anashukiwa kuiba vitu na vito vyenye thamani kutoka kwa nyumba ya bosi wake kabla ya kutokomea katika mtaa duni wa Congo, Kawangware.

Akinyi alikuwa mfanyikazi wa ndani katika nyumba ya raia wa kigeni kwa jumla ya miezi 15 kabla ya kutoweka na vito hivyo vikiwemo pesa taslimu Sh517,800, manukato, sarafu za dhahabu miongoni mwa vitu vingine.

“Tukio hilo lililoripotiwa Machi 11, 2025 katika Kituo cha Polisi cha Spring Valley, linaonyesha hadithi ya usaliti kutoka kwa mfanyakazi anayeaminika wa miezi 15, anayeaminika kuiba salama iliyojaa vitu vya thamani ikiwa ni pamoja na hati za kusafiria za familia, vitambulisho vya raia wa kigeni, dola za Marekani 4,000 [Sh517,800], sarafu za dhahabu, sanamu za Diwali, gari la kalamu, diski ngumu na diski nyingine,” DCI walisasisha.

Kijakazi huyo aliripotiwa kutotoka na vitu hivyo mnamo Machi 11 na baada ya kuripotiwa polisi, msako dhidi yake ulianzishwa na maafisa wa DCI ambao walimkamata akiwa amejificha eneo la Congo Maumau, mtaani Kawangware.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Kupitia ujasusi unaoongozwa na mahakama, Akinyi alifumaniwa katika maficho yake katika eneo lenye shughuli nyingi la Kawangware Congo Maumau, na kumaliza msako huo. Upekuzi katika makazi yake uligundua shehena ya vitu vilivyoibwa, kutia ndani noti 29 za dola mia moja, Rupia za India, manukato, na mikoba ya wanawake, vyote vilipatikana kwa mwajiri wake,” DCI waliongeza.

Makachero hao walidai kwamba mrembo huyo alikiri kufanya kosa la kutoweka na vitu vya aliyekuwa bosi wake na sasa anasubiri kufikishwa mahakamani kushtakiwa.

“Zaidi ya hayo, Akinyi alikiri kutupa sefu iliyoibiwa katika vilindi vya giza vya Mto Maumau. Kwa usaidizi kutoka kwa wapiga mbizi wa eneo hilo, wapelelezi walifanikiwa kuchota sefu hiyo kutoka kwenye mto na kuipata ikiwa tupu ndani yake. Akinyi kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi akishughulikiwa akisubiri kufikishwa mahakamani,” walisema.