Raila Odinga akutana na MCAs na viongozi wa Omogusii kutoka Nyamira na Nairobi

KIONGOZI wa chama cha ODM amefanya mkutano na wawakilishi wa wadi ambao wanatoka katika jamii ya Omogusii kutoka kaunti za Nyamira na Nairobi.

Akitoa sasisho kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Odinga alifichua kwamba mkutano huo pia uliwahusisha baadhi ya viongozi wa jamii ya Omogusii japo hakufichua ajenda ya mkutano huo.

Viongozi hao waliongozwa na mwakilishi wadi ya Kilimani kaunti ya Nairobi, Moses Ogeto na wenzake Duke Masir awa wadi ya Nyamira Township na George Morara kutoka kaunti ya Nyamira.

“Nilikutana na kundi la MCAs na viongozi wa jamii ya Kisii kutoka Kaunti za Nyamira na Nairobi. Tulijadili maeneo ya pamoja ya ushirikiano na maendeleo. Timu hiyo iliongozwa na George Morara, Duke Masira na Moses Ogeto,” Raila Odinga alifichua akiambatanisha na msururu wa picha kutoka kwa mkutano huo.

Mkutano huo unajiri siku chache baada ya Odinga kufokewa kwa hasira na mashabiki wa soka waliofurika katika ug awa Gusii kushuhudia uzinduzi wa jezi mpya za klabu ya jamii hiyo, Shabana FC.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Odinga aliandamana na gavana Simba Arati katika hafla hiyo ya Shabana FC iliyofanyika wikendi iliyopita, siku mbili tu kabla ya kutia Saini mkataba wa kufanya kazi Pamoja kati ya ODM na UDA.

Katika kile kilichoonekana kutowafurahisha wengi haswa kutoka jamii ya Omogusii, waliondoka kwa ghadhabu katika uwanja huo huku wakimtupia Odinga maneno wakimuita msaliti.

Tangu kutia Saini mkataba wa kufanya kazi Pamoja na serikali ya William Ruto, Odinga amepata wakati mgumu kuwaelewesha wafuasi wake ambao baadhi wanahisi kwamba aliwasaliti.

Hata hivyo, kabla ya kufokewa katika uwanja wa Gusii, Odinga alitetea muungano huo katika kaunti ya Migori ambapo alisisitiza kwamba hajasaliti mtu yeyote.

Kwa mujibu wa Odinga, hatua ya kuungana kwa ODM na UDA ni kwa manufaa ya wananchi wote, kauli ambayo imekuwa ikisisitizwa na rais Ruto katika maeneo mbalimbali.

Ruto anasisitiza kwamba kuungana na Odinga ni hatua moja katika safari ya kuleta maendeleo katika kila eneo la taifa lakini pia kutokomeza ukabila katika siasa za Kenya.