Mwanamziki mkongwe Lukas Mkenda maarufu Mr Nice amefichuwa kwamba wakati alifaulu katika maisha na pia kuanza maisha kama mzazi ililazimu apoteze marafiki wengine.

Ameeleza kwamba kuna baadhi ya vitu ambavyo alikuwa akifanya siku za zamani ambazo kwa sasa zimepitwa na wakati kwa hivyo hawezi kuendelea kuwa na marafiki wale wa zamani.

Kwenye mahojiano na mwanahabari ameeleza kwamba marafiki zake wa zamani wanamuona kama mtu ambaye ameeishiwa kwa kuacha kujishugulisha nao na kubadilisha mienendo ya maisha yake.

"Wengine wanasema Mr Nice ameeishiwa, ndo maana siku hizi anajifanya amepunguza marafiki, la, sasa nina watoto watatu, huo muda sikuwana na watoto. nilikuwa mtu ivoivo. Kuna mahali lazima maisha ibadilike tu, utake usitake," alisema Mr Nice.

'Mimi sasa hiviu niko over 40. Kwa sababu kama nafikisha 47 si karibu 50 Mungu akipenda. Maisha ambayo nilikuwa naishi zamani siwezi nikaishi sasa hivi. Kwa sasa unaeza nipata tu mtaa niko mguu sasa hapo watu wanasema ameishiwa siku hizi ata gari ni kama ameuza au hana pesa ya mafuta. Hizo zote zanaongelewa," aliendelea kueleza mwanamziki huyo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mr Nice ameeleza kwamba ana lengo ambalo humufanya wakati mwingine kutembea kwa miguu na kuacha gari lake. Kulingana na yeye moja ya lengo hilo ni anagalau kuafikia watu na kujua hali zao. Pia ameeleza kwamba watu wanapo muona akiwa bila gari wanafaa kushukuru maana ndiyo nafasi pekee ya kukutana na yeye angalau wasalimiane.

'Wewe unataka unione kwa gari kila saa, nimekwambia mimi ni mlemavu. mimi sikuzaliwa kwenye gari. Nikitembea kwa gari utaniona sa ngapi? Wewe shukuru nikitembea kwa miguu maana umeniona ata unisalimie,"alieza.

Mwanamziki huyo amesistiza kwamba kwa kadri umri unavyosonga ndo pia inampasa mtu kuacha tabia za ujanani kwa sababu majukumuu pia huongezeka.

"Maisha yamebadilika, nishakuwa mtu mzima na familia. Nina mahitaji wale marafiki ambao wanasema Mr Nice ameeishiwa waelewe hilo. Adui ni rafiki. Hakuna mtu wa mbali anaeza sema Mr Nice ameishiwa. Hata mtu wa mbali haezi kuja kukuibia maana hajui kiko wapi hicho kitu ni rafiki,' alieleza zaidi mwanamziki huyo.

Mr Nice ni msanii mkongwe wa Tanzania na mmoja wa waimbaji maarufu zaidi katika Afrika Mashariki akitawala muziki wa Afrika Mashariki mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakiwa pamoja na Jose Chameleone wa Uganda na Jua Cali wa Kenya.