Khaligraph Jones na Kaa la Moto
Mwanamuzi mkongwa maarufu nchini Tanzania Profesa Jay ameorodhesha wasanii wawili wa nchini Kenya kuwa miongoni mwa wasani ambao anawapa heko.

Profesa kwenye kikao na wanahabari ameweka wazi kwamba anawatambua wananamziki kadhaa ambao wanaendelea kusongesha mziki wa Afrika Mashariki kwenye hatua nyingine.

Miongoni mwa wasanii maarufu ambao amewaorodhesha hapa nchini Kenya ni pamoja na Khaligraph Jones ambaye pia anajulikana kama Papa Jones na vilevile mwanamuziki wa Mombasa Kaa la Moto.

"Msani wa Kwanza ambaye kiukweli namuenzi ni Dizastar Vina, ni msani ambaye anatumia aklili kubwa kwenye uimbaji wake. Ashawahi kuimba na msanii Kaa la Moto wa Mombasa Kenya na pia ni msanii mzuri ," alieleza.

kuna Mex Cortez na Khaligraph Jones, Marifa, hawa ni vijana ambao wanafanya vizuri kimuziki na kuunganisha kizazi chetu mpaka kwa kizazi kingine. Kwa hivyo kuna timu kubwa ambayo inaimba mziki mzuri na inanifurahisha," aliweka wazi mwanamziki huyo.

Wakati akizungumza pia ameelezea kwamba iwapo mwanamziki anataka kusonga katika hatua nyingine ni lazima atengeneze urafiki mzuri na watu na pia vyombo vya habari.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Migogoro ipo ila kuna kutegemeana, Upande mmoja wasanii, upande mwingine vyombo vya habari na upande mwingine mashabiki. Msanii kuwa na ugomvi na media ni kitu kibaya sababu inamrudisha nyuma msanii. Lakini pia media kuwatenga wasani inaharibu kazi za watu wengi, na vijana wengi wamejiajiri kupitia muziki. Wakati huo pia msani kuwa na uwadui na mashabiki ni kitu kibaya maana ndio wanakufanya ufike ulipo, aliweka wazi.