
JIJI la Eldoret sasa ni jiji lililokamilika shukrani kwa uongozi wa kaunti ya Uasin Gishu ambao umekuwa ukijibiisha kuliboresha katika hadhi hiyo ambayo lilipewa miezi 6 iliyopita.
Hatua ya hivi punde ya kuboresha hadi hiyo ni kuwekwa kwa taa za trafiki katika baadhi za barabara jijini humo.
Akithibitisha kuwekwa kwa taa za trafiki, gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii alichapisha msururu wa picha akionesha taa hizo zikiendelea kuwekwa katika barabara kuu ya jiji hilo.
“Kuweka mji wetu katika udhibiti! Ufungaji wa taa za trafiki unaendelea,” Gavana Bii alisasisha.
Mji wa Eldoret ulikabidhiwa hadhi ya kuwa jiji la 5 la Kenya mwezi Agosti 2024 katika hafla ambayo iliongozwa na rais William Ruto.
Tukio hili la kihistoria, ambalo pia lilipambwa na Mabingwa wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, linapatana kikamilifu na ajenda ya maendeleo ya serikali, ambayo inalenga kuendeleza ukuaji wa kikanda, kuboresha miundombinu na kuimarisha uwezo wa kiutawala.
Mwinuko wa hadhi ya jiji unatarajiwa kufungua fursa muhimu za uwekezaji na kukuza mazingira ya kiuchumi yenye nguvu zaidi, kuunga mkono kikamilifu dira ya kubadilisha miji na majiji yetu kuwa vitovu vya maendeleo.
Hadhi mpya ya Eldoret kuanzia sasa itaigeuza kuwa kituo chenye nguvu cha ukuaji wa uchumi kwa Kambi ya Kiuchumi ya North Rift (NOREB) na ishara ya amani.
Kama lango la majimbo ya kaskazini mwa Sudan, Ethiopia, na kwingineko, mji mpya—wa tano wa Kenya—pia utaunganisha mataifa haya na bandari ya Mombasa, na kuwa kitovu muhimu cha shughuli za ujasiriamali zenye umuhimu mkubwa kwa mtaa mzima.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!