Msanii maarufu nchini Kenya Willy Paul amepinga madai kwamba anachukiwa sana Watanzania na wasanii wa nchi hiyo jirani.

Mwanamuziki huyo ambaye pia ameandika kwenye mtandao wake wa facebook akisema kwamba yeye anaapenda watanzania wote wala hajakosana nao kwa vyovyote vile.

Msani huyo amesisitiza kwamba Kenya na Tanzania ni Mandugu na wanafa kuungana kwa pamoja. Hata hivyo msani huyo pia ameeleza kwamba hapoendi dharau huku akieleza kwamba msani wa Tanzania alikuja nchini na kumuonesha dharau nyumbani kwao.

"Ndugu zangu TZ, msidanganywe eti nina chuki na nyinyi au wasanii wenu. Sisi sote mandugu na kila mmoja anamhitaji mwingine kile ambacho sipendi ni dharau. Msanii wenu alikuja kuniletea dharau hapa nyumbani ... nikakataa na bado nitakataa tu," aliandika msanii huyo.

"Akabadilisha story na kusema kuwa nawachukia watanzania. mimi sina chuki na watanzania. Nawapenda wote ndugu zangu na dada zangu," alisema Willy Paul.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mwanamuziki huyo wa Kenye Mwenye Kibao kinachovuma cha 'KEKI' ambacho alimushirikisha 'Bahati Kenya' amefichua kwamba siku za hivi karibuni kabla Jumaa halijakamilika atakuwa ameachia kibao kipya akimushirikisha mwanadada kutokea Tanzania ambaye anajulikana kwa jina la usanii Phina.

"Nina wimbo na msani aliyefanikiwa Phina ambao utakuwa unatokea hii wiki,' aliandika Willy Paul Kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Hii sio Mara ya kwanza Willy Paul kushirikana na wasanii wa Tanzania kwenye kazi ya mziki. Paul aliwahi kufanya Kolabo na wasani wa Tanzania kama vile Mario, Jux miongoni mwa wengine.

Baada ya kutokea mtafaruku kati ya Willy Paul na Diamond siku za nyuma, msani Willy Paul ameamua kujituma na kuachia ngoma moja baada ya nyingie. Mwezi jana msani huyo aliwachia ngoma mbili kwa pamoja zote wakishirikiana na msanii mwenzake wa Kenya ''Bahati Kenya".