Mwanamuziki wa Kike Phina kutoka nchini Tanzania amejitokeza waziwazi na kuomba msamaha kwa niaba ya msanii wa Kenya Willy Paul kwa wananchi wa Tanzania.
Phina aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akiwataka wananchi wa Tanzania kumusamehe msanii huyo kwa yote yaliyotekea nyuma.
Phina na Willy Paul Msafi wanatarajiwa kuachia kolabo yao hivi Karibuni baada ya wawili hao kuingia studio wakiwa hapa nchini Kenya.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Phina ameandika Y' all ready? @willy,paul.msafi kuna kale kamsemo "Samehe mara saba sabini" wabongo kamewapitia wapi.
Phina ambaye pia anajulikana kama Saraphina, majina yake kamili ni Sarah Michael Kitinga kwa sasa ana umri wa miaka 29, ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo.
Nyimbo zake kama Rara, Superwoman, Manu, Sponsor, Sisi Ndo Wale na Upo Nyonyo ambao ulipangwa nambari 62 na tovuti ya muziki ya Nigeria NotJustOk kwenye orodha yao ya nyimbo bora za Tanzania kutoka mwaka 2012 hadi 2022.zimemfanya kuwa jina maarufu nchini Tanzania.
Katika kipindi chote cha kazi yake, Phina ameshirikiana na wanamuziki mbalimbali maarufu ikiwa ni pamoja na Jux, Otile Brown, Jay Melody na Ruby.
Mwanadada huyo ameamu kuomba msamaha kwa watanzania akihofia kwamba huenda wenyeji wa nchi hiyo wasiukumbatie wimbo wao ambao unatarajiwa hivi karibuni kutokana na mvutano uliofanyika kati ya Wily Paul na nyota wa Tanzania Diamond Platinumz.
Wasani hao wawili walikosana kwenye Furaha Festival ambazo zilikuwa zimeandaliwa hapa nchini. Mvutano ulitokea wakati wa kupanda jukuani kuhusu ni yupi apande wa kwanza kati ya Diamond na Willy Paul.
Willy Paul alifika kwa wakati mmoja na kutaka kutumbuiza kabla ya Diamond. Alikuwa tayari na wachezaji wake na alisisitiza itifaki ifuatwe kama ilivyokubaliwa awali. Hali hii ilizua sintofahamu kati yake na timu ya usimamizi ya Diamond inayoongozwa na SK Sallam kwani msani huyo wa wasafi pia alitaka kutumbuiza wa kwanza.
Willy Paul alifanikiwa kupanda jukuani wa kwanza, ila kutokana na mvutano huo wa muda mrefu ulimfanya Diamond kuondoka kabla ya kutumbuiza umati.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!