
ASKOFU wa CITAM aliyeongoza ibada ya wafu kwa marehemu aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC ameonyesha kutofurahishwa na jinsi baadhi ya watu wamekuwa wakidhihaki msiba wa Chebukati.
Akizungumza Jumatano katika ibada hiyo ya wafu, askofu huyo alisema kwamba si vizuri hata kidogo kwa watru kuchukulia suala la familia inayoomboleza kumdhihaki mpendwa wao.
“Familia ambayo imeketi mbele yetu mahususi imepata pigo kubwa kwa kufiwa na mpendwa wao. Na ndio wakati wa msiba ambapo familia hii imeshambuliwa na Wakenya. Mambo yanmesemwa, hukumu zimetolewa kwao na siwezi hata tafakari ni nini wamekipitia,” Askofu huyo alisema.
Mchungaji huyo alitoa wito kwa Wakenya akisema kwamba mambo ambayo baadhi yao wamekuwa wakiendeleza katika mitandao ya kijamii kudhihaki na kukejeli msiba wa Chebukati si jambo la kufurahikiwa bali ni la kununiwa na kukemewa.
‘Ningependa kuwaambia Wakenya wenzangu, hii sio poa. Si jambo la kumpendeza Mungu, si tamaduni ya Kiafrika na hata sio utu. Hatuwezi jificha nyuma ya mitandao ya kijamii kushambulia familia ambayo tayari inaomboleza.’
“Ni jambo la kutamausha, ni vigumu na inachukua kila kitu kutoka kwako kiasi kwamba Kauli pekee unataka kusikia ni ‘pole’. Lakini kwa bahati mbaya huu ndio wakatibaadhi ya watu wanachukua mawe na kuyarusha kwa wale wanaoomboleza,” aliongeza.
Askofu huyo alihubiri akisema kwamba wale wanaokejeli na kudhihaki kifo cha Chebukati wanapaswa kujua kwamba kufanya hivyo ni kinyume na mila na tamaduni za Waafrika.
Kwa mujibu wake, tamaduni za Kiafrika zinataka marehemu kumiminiwa sifa hadi anapoingia kaburini, bila kujali iwapo alikuwa mzuri au mbaya kwani marehemu hasemwi kwa njia hasi.
“Hata kama tunajua kwamba huyu mtu hakuwa mzuri, tunajifanya tu kusema jinsi alivyokuwa mtu mzuri. Hiyo ndio tamaduni ya Afrika. Si vizuri kudhihaki kifo chake,” askofu huyo alihubiri.
Aliendelea kuishauri familia ya marehemu Chebukati kwamba huu ni wakati wao kujikusanya upya ili kuchanganua upya nafasi yao na uhusiano wao na Mungu.
Chebukati anatarajiwa kuzikwa wikendi hii ya Machi 8 nyumbani kwake katika uliokuwa mkoa wa Magharibi mwa Kenya.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!