
MCA wa Kileleshwa, Robert Alai amewasilisha mswada katika bunge la kaunti ya Nairobi akilenga kushinikisha vifaa vya uchukuzi jijini kama mikokoteni na wheelbarrow kusajiliwa rasmi.
Katika mswada huo ambao unatarajiwa kujadiliwa katika bunge la kaunti hiyo, Alai alisema kwamba kusajiliwa kwa mikokoteni, wheelbarrow na vifaa vingine vya kusukumwa kutaleta utulivu katika uchukuzi wa mizigo jijini.
“Mpango huu unalenga kushughulikia msongamano unaoongezeka na wasiwasi wa usalama unaosababishwa na matumizi makubwa ya njia hizi za usafiri, ambazo zinachangia asilimia 45 ya uhamaji katika kaunti, kulingana na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa,” sehemu ya maelezo kuhusu mswada huo yalisema.
Ikiwa mswa utapata bungeni, mikokoteni na wheelbarrow zitasajiliwa na NTSA na kupewa namba za usajili huku wanaoisukuma wakilazimika kuvaa reflective jackets.
“Hoja hiyo inataka utoaji wa nambari za kuakisi kwa usafiri wote usio wa gari, matumizi ya lazima ya jaketi za kuakisi na waendeshaji, na mahitaji kwa waendeshaji kupata bima ili kulinda dhidi ya ajali na uharibifu wa watu wengine.”
Hatua hizi zitahakikisha nidhamu ya njia, kuimarisha usalama barabarani, na kutoa mfumo kwa waendeshaji kupata maarifa muhimu ya usalama barabarani.
Kipindi cha miezi sita bila malipo kitatolewa kwa utiifu pindi miongozo itakapotekelezwa, kwa ushirikiano na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA).
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!