Peter Kaluma, mbunge wa Homa Bay Town

MBUNGE wa Homa Bay mjini Peter Kaluma ameomba desturi ya kutahiri wanaume nchini Kenya kupigwa marufuku akisema kwamba suala hilo halina umuhimu wowote katika maisha na mwili wa mwanamume.

Kupitia ukurasa wake wa X, Kaluma alisema kwamba suala la kutahiri watoto wa kiume lilikuwa linafanywa tu na Abraham kwenye Biblia enzi za zamani kwa sababu yeye alikuwa anaishi jangwani pasipo na maji.

Mbunge huyo alisema kwamba kutahiri wanaume ni sawa na kuhujumu haki zao za kiume, akidai kwamba ni desturi isiyo na maana yoyote.

Kaluma alisema kwamba hakuna mnyama wa kiume hata mmoja ambaye anatahiri isipokuwa tu mwanadamu, akitolea mfano kwamba hata punda hawatahiri na wanaishi sawa tu!

“Acha kutahiriwa. Tohara ni kukata wanaume. Punda hawatahiri. Wanyama wote hutahiriwa isipokuwa wanadamu wachache ambao wamedanganywa kwamba wao ni wajukuu wa Abrahamu, mtu aliyeishi jangwani bila maji!” Kaluma alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Licha ya maoni yake kuonekana kuwa na maana, baadhi ya watumizi wa X walionekana kukinzana naye, wengine wakisema kuwa mwanamume kutahiriwa humdumishia usafi wan yeti yake.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

@nyawade_rodgers: ‘Hapa uko pekee yako. Tohara ni jambo bora zaidi ambalo mwanaume anaweza kujifanyia mwenyewe.”

@__Munguti: “Je, unasema Bwana alikuwa mwendawazimu alipoamuru kutahiriwa? Hivi majuzi, inaonekana kama umetweet ili kugusa ego yako. Ikiwa hujakatwa, hiyo ni biashara yako-waache wale wanaotaka wafanye mambo yao. Jiwekee!”

@justinawamae: “Nitawaongoza wanawake kupinga maoni yako.”

@mtume_tyson: “Unapoanza kwenda kinyume na neno la Bwana, maana yake umepoteza mwelekeo... unaelekea uharibifu.”

@MaishmainaB: “Tohara ya wanaume sio tu kukatwa, ni mengi yanayoambatana na.haki ya kupita.kama jamii hufanyi mazoezi waache wanaofanya hivyo.unachoamini ndicho unachopata.”

@didacushill: “Ngozi ya mbele ndiyo sababu ya watu wengi kuwasiliana na VVU. Wakati wa kujamiiana, ngozi ya mbele inasukumwa nyuma ili kufichua glans ya uume. chini ya msukumo mkali, msukumo huu husababisha machozi kwenye sehemu ya govi ya kugusana na glans. Hii inaweka wazi mwathirika kwa maambukizo kwa nafasi ya 80%. Acheni uwongo kwa luos, watakufa kama panya.”