Diamond Platinumz ambaye ni mwanamuziki maarufu wa bongo kutokea nchini Tanzania ameonesha kutoridhishwa na juhudi za serikali kwenye suala zima la kukuza taaluma ya muziki.
Diamond alikuwa akizungumza baada ya mashindano ta trace awards yaliyofanyika zanzibar ambayo yaliwaleta pamoja wanamziki mbalimbali.
Mwanamziki huyo ambaye pia ni mshindi wa tuzo za Trace kama msanii bora wa Africa, alionesha kukosa imani na mazingira kwa wasani humo nchini.
"Lakini kitu cha kuomba mimi, natsaka niombe kitu kimoja kwa serikali watujengee arena, ukiangalia Trace wamepata shida sana, wanatengeneza stage inadondoka, sio mazingira rafiki, watujengee arena ili tufanye vitu vizuri," alisema Diamond
Vitu kama hivyo vikifanyika vinakuza utalii. Tazama wasanii wa Tanzania walivyoonekana wengi, naamini kuna wengine tulikuwa tufaamiki sasa tumefahamika, hali imeongezeka. Serikali najua inatufanyia mambo mengi lakini trunaitaji arena," alisistiza rais huyo wa Wasafi.
Mwanamziki huyo wa bongo alielekeza maombi yake moja kwa moja kwa rais wa muuungano wa Tanzania rais Samia Suluhu akitaka awakumbuke wanamziki. kulingana naye viwanja nya mpira viko katika kila mkoa toafauti kabisa na eneo la wasanii.
Tunahitaji arena, tumekuwa tukisema hili miaka na miaka. mheshimiwa rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, najuwa wewe msikivu, wewe mtendaji, wewe mwenye huruma, ebu tuhurumie na sisi wanamziki tupate Arena. wacha za mpira kiasi, viwanja wananavyo kila mkoa. kila mkoa kuna kiwanja, sisi arena moja kweli ndio tutatia asara nchi. tuseme kupitia sisi ndo nchi itafilisika," alisema Diamond kwa machungu.
Msanii huyo pia anaamini kwamba kutokana na hilo taifa litapata kuvutia watalii, na arena hiyo itatumika kwa shughuli zingine ambazo pia zitasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa njia moja au nyingine.
Tanzania ikipatikana arena, hapo kutafanyika mikutano, netball, basket ball, makongamano, show, events, harusi, watusaidie hapo. watu wa inje wakija kufanya mikutano," alieza
Mshindi huyo wa tuzo ya Trace amesistiza kwamba Tanzania ina vipaji vingi vya kimuziki ila mazingira yanawapiga chenga kwa wale wachangaa, wanashindwa kuchagua kati ya kwenda au kurudi kwenye mziki.
'Mziki wa Tanzania una nguvu kubwa sana ila wanakosa vitu kama hivili ili uonekane ukubwa wake, ... Tazama akina Nandy, kina Harmonize, zuchu, watu wanashambulia lakini haya mazingira? kuna wengine je wataweza, watarudi mara ya pili. ndo waweze kurudi mara ya pili inalazimu tuwatengenezee mazingira. alisema Platinumz.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!