Mfanyibiashara wa magari, Khalif Kairo

JOSEPH Wambui, maarufu kama Khalif Kairo amefichua kwamba Wahisani walimchangia takribani shilingi laki 8 mwezi jana alipoomba msaada mitandaoni.

Mfanyibiashara huyo wa kuuza magari alifichua takwimu hizi wakati wa mahojiano ya kipekee kwenye runinga ya Y254 na nguli Brian Sakwa.

Kairo alilenga kujibu swali la uvumi kwamba alitumia michango ya Wakenya kufadhili safari yake kwenda Dubai, akisema kwamba kutoka kwa michango hiyo alitumia Sh20,000 pekee.

Alisema kwamba salio jingine lilienda moja kwa moja katika mfuko wa kuifufua kampuni yake ya kuuza magari – Kai&Karo, akiahidi kuja kutoa maelezo kamili ya jinsi safari yake ya Dubai ilitokea.

“Wakenya walinichangia takribani 700,000 au 800,000 na 95% ya hizo pesa ilienda kwa kampuni yangu. Unajua nikiwa Dubai niliona watu wakisema ooh unatumia pesa zetu za paybill, si kweli.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Kusema kweli siku moja nitasimulia hadithi jinsi nilienda Dubai, ni muujiza kamili. Nilichangiwa 800k, na asilimia 95 ikaenda kwa kampuni, mimi nilitumia tu Sh20,000,” aliongeza.

Katika hii asilimia 95, Kairo alieleza kwamba zilitumika kuwalipa baadhi ya wafanyikazi wake ambao walikuwa wengine wanadaiwa nyumba na zingine zikamaliza bili katika afisi zao.

“Salio jingine tuligawanya kwa kampuni kwa sababu wengi wa wafanyikazi wangu walikuwa wanapitia wakati mgumu kweli. Watu walikuwa wanadaiwa kodi za nyumba hivyo ilitubidi tukalipia baadhi kodi za nyumba, zingine tulilipia matangazo yetu, zingine tulilipa bili za stima… kwa hivyo shukrani sana Wakenya mlifanya kazi kubwa kuinusuru kampuni wakati nilikuwa kwenye kipindi change kigumu zaidi,” Kairo alimaliza.