KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Februari 5.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Nandi, Kisumu, Kakamega, Kwale na Kilifi.

Katika kaunti ya Kilifi, sehemu za maeneo ya Kikwete Road na Milimani zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Moi University na Ollessos Technical katika kaunti ya Nandi yataathirika kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Eneo la Soko ya Nyahena katika kaunti ya Kisumu litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Soko la Ematiha katika kaunti ya Kakamega litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Mvindeni katika kaunti ya Kwale zitakosa umeme kati ya sa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Kokotoni katika kaunti ya Kilifi pia litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.