SHIRIKA la ndege la Kenya, limetoa taarifa kuhusu video ambayo imekuwa ikizua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii ya abiria mmoja akikorofishana na wafanyikazi wa shirika hilo jijini Nairobi.
Video hiyo ilichapishwa na raia mmoja anayekisiwa kutoka Nigeria ambapo alilalamika kwa sikitiko kubwa Mnigeria huyo mwanamke aliburuzana na wafanyikazi wa ndege Kenya.
“Uangalifu wetu umetolewa kwa visa kadhaa vya unyanyasaji wa kinyama kwa abiria wa Nigeria huko Nairobi na @KenyaAirways. Kesi ya Bi. Omisore G. ambaye alisafiri kwa ndege kutoka Manchester hadi Lagos, akiunganisha-Man-CDG-NBO-LOS, lakini ikakataliwa kuabiri Nairobi kwenye mkondo wa 2 wa tikiti sawa,” jamaa huyo kwa jina Tunde Moshood alisema.
Ni kutokana na chapisho hili ambapo Kenya Airways waliamua kujibu na kuelezea muktadha mzima wa tukio hilo wakifichua kwamba video hiyo haielezei vyema tukio kwa ukamilifu.
KQ walieleza kwamba abiria huyo ndiye alizua mfarakano ambapo anadaiwa kutoa sodo 3 zilizotumika na kuwatupia wafanyikazi wake katika kiti cha kuhudumia wateja.
“Kwa muktadha: Mgeni huyo alikuwa akisafiri kutoka Lagos kwenda Nairobi, Paris, na Manchester. Alipofika Nairobi kwa ndege yake ya kuunganisha (Nairobi-Paris), iligunduliwa kwamba hakuwa na Visa ya SCHENGEN, ambayo ni sharti kwake kuingia katika Nchi yoyote ya Umoja wa Ulaya.”
“Alipewa njia mbadala ya kusafiri kupitia London na kuendelea hadi Manchester, ambayo alikataa. Baada ya uchunguzi zaidi, tumegundua kuwa video haitoi muktadha kamili.
“Bila kufurahishwa na chaguo hili, mgeni alidai malazi, ambayo Kenya Airways haitoi katika hali ambapo kukwea kumenyimwa kutokana na mahitaji ya viza. Ni jukumu la abiria kuhakikisha wana nyaraka zinazohitajika kwa safari yao.
“Katika hali ya kutatanisha, mgeni alianza tabia isiyofaa kwa kuvua na kuwarushia wafanyakazi wetu pedi 3 zilizotumika,” KQ walitoa sasisho kupitia X.
KQ walikashifu vikali tabia hiyo ya abiria na kusema kwamba ni vyema watu wajue muktadha mzima kabla ya kuanza kuhukumu.
“Tunalaani vikali tabia hiyo. Ingawa tumejitolea kutoa huduma ya kipekee, tunatarajia mwingiliano wote uwe wa kuheshimiana. Wafanyakazi wetu wanastahili kufanya kazi katika mazingira salama na yenye heshima, na hatuvumilii unyanyasaji wowote kutoka kwa wafanyakazi wetu au wageni.”
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!