Rais William Ruto wa Kenya na rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi waliandaa kikao cha pamoja mjini Kairo siku ya Jumatano Januari 29,2025 ili kujadili masuala ambayo yanaazimia kuleta mshikamano wa pande zote mbili na kudumisha amani kwa mataifa hayo yote mawili.
Baada ya mkutano huo, Ruto alielezea kwa urefu kile ambacho walijadili kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii akifafanua kile ambacho walijadili na mikataba ambayo walitia sahihi ili kudumisha utangamano na mshikamano wa mataifa haya mawili.
Baadhi ya mikataba iliyotiwa sahihi ni mkakati wa pamoja na ushirikiano wa mataifa yote mawili( Joint Declaration for strategic and comprehensive partinership) ambao wote walikubaliana kuwa utakuwa wa manufaa kwa nchi zote mbili.
Rais alikariri kuwa makubaliano hayo yatapanua wigo wa ushirikiano pamoja na makubaliano mengine kumi na mawili(12) ambayo yanalenga biashara, uwekezaji, elimu, utafiti na teknolojia.
Hatua hii kulingana na Ruto inalenga kuzipa nchi zote fursa sawa.
Viongozi hao pia walichukua muda wao kulivalia njuga suala la usalama ukanda wao hasahasa vita vinavyoendelea Somalia,Sudan na mashariki ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ruto alirai ushirikianao wa dharura ili kumaliza vita hivyo ambavyo vimeathiri maisha ya watu,kusababisha vifo ,kuhama kwa watu na kupoteza mali zao.
'Vita Afrika vimesababisha watu kupoteza maisha, makao na uharibifu wa mali na vitu vyote vya thamani kutokana na hili ni jambo la dharura tuje pamoja tushirikiane ili tumalize vita hivi na mzozo huu wa bunduki na turudishe watu wetu katika hali ya salama hasahasa Sudan, Somalia na mashariki ya Kidemokrasia ya Kongo ili bara la afrika litulie na lipate amani'.
Ruto alimshukuru Eli -Sisi kwa kujitolea kwake kuhakikisha kuwa amani inarejea katika taifa la Sudan, Somalia na mashariki ya nchi za milki za kiarabu( middle East).
Mkutano huo ulifikia kilele chake katika makao makuu mikutano ya taifa ya rais mjini Kairo ambapo viongozo wote wliahidi kushirikana ili kumaliza vita afrika na hata nje ya afrika.
Mkutano huo wa marais hawa wawili uliashiria mwanzo mpya wa ushirikiano baina ya nchi ya Misri na Kenya mataifa yote mawili yakiweka ahadi pana kuwa watashirikiana na kuhakikisha kuwa biashara,uvumbuzi wa teknolojia na ushirikiano wa amani ya kudumu inatekelezwa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!