MWANAMUME mmoja mwenye umri wa miaka 20 anashikiliwa na polisi baada ya kumuua mwanawe mwenye umri wa miezi 8 kwa kumketisha barabarani na kumkanyaga kwa gari baada ya kugombana na mkewe.
Kwa mujibu wa jarida la News 4 Jax, baba huyo wa kutoka jimbo la Florida nchini Marekani alimketisha mwanawe katikati ya makutano ya barabara yenye shughuli nyingi kabla ya kuendesha gari juu yake kwa kasi.
Justin Golden, mwenye umri wa miaka 20, alikuwa akiendesha gari katika makutano ya barabara za Lenox na McDuff huko Jacksonville mwendo wa saa 11 asubuhi Jumamosi, wakati inadaiwa aligombana na abiria huyo - ambaye anaaminika kuwa mama wa mtoto huyo, News 4 Jax inaripoti.
"Dereva alisimamisha gari kwenye makutano, akafungua mlango na kumweka mtoto chini," Ofisi ya Sheriff ya Jacksonville ilidai.
"Dereva alianza kuondoka eneo hilo na gari likamgonga mtoto."
Baada ya kumuua mwanawe, jamaa huyo alitaka kukimbia eneo la tukio, lakini maafisa waliweza kumpata haraka na kumweka chini ya ulinzi.
Wakati huo huo, wahudumu wa afya walimkimbiza mtoto huyo hospitalini, ambapo madaktari walitangaza kuwa mtoto huyo amefariki.
Polisi wa Jacksonville wanaendelea kuchunguza tukio hilo, na bado hawajafafanua iwapo Golden alimkimbia mtoto huyo kwa makusudi.
'Sisi, pamoja na washirika wetu katika Ofisi ya Mawakili wa Serikali' hatutasimama kwa lolote ili kupata haki kwa mtoto huyo,' ofisi ya sheriff ilisema.
Golden sasa anakabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia, kuua kwa njia ya gari na kukosa kutoa msaada, na anazuiliwa katika Jela ya Duval County bila kifungo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!