ZAIDI ya walimu 189,000 walituma maombi ya kupandishwa vyeo kwa tume ya kuajiri walimu TSC licha ya tume hiyo kutangaza nafasi 25,288 pekee wiki mbili zilizopita.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kwenye gazeti la Business Daily, TSC ilibaini kupokea maombi hayo ambayo ni mara 8 zaidi ya nafasi za kupandishwa vyeo walizotangaza.
Katika notisi ya awali, TSC ilikuwa imeorodhesha nafasi 9,179 za kupandishwa vyeo kwa walimu wa shule za upili na nafasi zingine 16,109 kwa walimu wa shule za msingi.
Hata hivyo, takribani maombi 189,000 yalitumwa na walimu wa vitengo mbalimbali kutoka kote nchini.
Itakumbukwa katika mgomo wa waalimu wa shule za upili KUPPET, moja ya matakwa yao yalikuwa kutaka tume ya TSC kuwapandisha vyeo angalau walimu 130,000 ambao walidai kwamba walikuwa wamekwama katika ngazi moja ya kikazi kwa muda mrefu.
“Kuna changamoto kubwa ya kukwama kwenye ngazi moja ya kitaaluma kwenye fani ya ualimu. Hiii nadhihirika wazi kutokana na idadi kubwa ya walimu ambao hawajawahi pandishwa vyeo kwa zaidi ya miaka 5,” alisema katibu mkuu wa KUPPET, Akelo Misori.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!