Siku ya Jumanne, Januari 21, bintiye mke wa Guardian Angel Esther Musila, Gilda Maua Naibei aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Mtoto
huyo wa pili wa Bi Musila alisherehekea kutimiza miaka 31 na mamake alitumia
fursa hiyo kumsherehekea kwa jumbe nzuri.
Bi Musila alimtakia bintiye siku njema ya kuzaliwa na kumuombea ulinzi wa Mungu.
"Unapoongeza mwaka mmoja zaidi, na ufurahie kuwa wewe mwenyewe. Nakutakia furaha, amani, upendo na kicheko. Ninaomba kwamba Mwenyezi aendelee kukuongoza na kukulinda siku zote za maisha yako,” Bi Esther Musila alimwandikia bintiye.
"Na ufuate tamaa ya moyo wako na kukabiliana na changamoto za maisha zisizoepukika kwa udadisi, sio hofu. Heri ya miaka 31 kwako, mtoto wangu. Upendo mwingi, "aliongeza.
Katika ujumbe mwingine, mkewe Guardian Angel alimhakikishia binti yake jinsi anavyojivunia yeye.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 54 pia alimhakikishia Gilda upendo mkubwa alionao kwake.
“Maua nakutazama sioni jinsi muda ulivyokupita. Miaka 31 iliyopita, nilibarikiwa kupata mtoto wa kike mrembo zaidi. Huenda nisiweze kukubeba tena mikononi mwangu, lakini nitakubeba moyoni mwangu kila wakati. Nitajaribu na kukuheshimu kuwa wewe ni mwanamke mzima sasa, lakini utakuwa msichana wangu mdogo kila wakati. Leo, unasherehekea siku yako ya kuzaliwa, na ninajivunia mafanikio yako madogo na makubwa, na tunamshukuru Mungu kwa hilo. Heri ya siku ya kuzaliwa kwako, na ninakutakia baraka za Mungu, afya njema, na marejeo mengi ya furaha. Heri ya siku ya kuzaliwa, Maua. Nakupenda,” aliandika.
Baba wa kambo wa Gilda, Guardian Angel pia alichukua fursa hiyo kumsherehekea, kumtakia mwaka mwema ujao, na kumhakikishia upendo wake mkubwa kwake.
"Siku ya Kuzaliwa yenye Furaha, Baraka kwako @onlygilda. Utakuwa mwaka mzuri kwako. Upendo mwingi,” Guardian Angel aliandika.
Gilda ni mmoja wa watoto watatu wa Esther Musila kutoka kwa ndoa yake ya awali. Ana watoto wengine wawili wa kiume, Jamal na Kim Naibei.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!