IDARA ya DCI imevunja kimya baada ya maafisa wake kushambuliwa na umma katika kaunti ya Kirinyaga walipoenda kumtia mbaroni mshukiwa mmoja.


Kupitia picha na video zilizoenezwa mitandaoni, maafisa hao waliokuwa ndani ya gari dogo walifumaniwa na umma uliokuwau mejaa ghadhabu wakitishia kuliteketeza gari lao.


DCI kupitia ukurasa wao wa Facebook walitoa taarifa kuhusu tukio hilo wakionya umma vikali na kusema kwamba kujaribu kuzuia makachero dhidi ya kutekeleza majukumu yao ni kosa kubwa kisheria.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Walisema kwamba maafisa wake walimusurika kushambuliwa na umma, shukrani kwa maafisa kutoka kituo cha polisi kilichopo karibu na eneo la tukio, chifu na wazee wa nyumba kumi.


“Maafisa hao walikuwa wametumwa na Afisa wa Upelelezi wa Jinai wa Kaunti Ndogo kumsaka mshukiwa aliyetoroka.”


“Kundi la watu wenye ghasia, hata hivyo, walikusanya vikosi na kuwashambulia maafisa waliokuwa kwenye gari la serikali nambari ya usajili KBZ 684Y, wakitishia kuiteketeza iwapo hawatamwachilia mshukiwa.”


“Shukrani kwa polisi wa eneo hilo, chifu wa eneo hilo na wazee wa Nyumba Kumi, ambao walishinda hali ya wasiwasi na kuwezesha kuwekwa kizuizini kwa mshukiwa,’ DCI walisema.


“DCI inatahadharisha umma kwamba kuwazuia maafisa wa polisi katika kutekeleza majukumu yao ya kikatiba ni kosa kubwa la jinai, na mbaya zaidi ni jaribio lolote la kusaidia kutoroka kwa mhalifu au mfungwa,” waliongeza.


Kisa hicho kinajiri wakati ambapo serikali imekuwa ikilaumiwa dhidi ya msururu wa utekaji nyara ambao umekuwa ukifanyika nchini.