RAIS WILLIAM RUTO alizua vichekesho Alhamisi wakati wa uzinduzi wa chuo cha mafunzo ya uuguzi cha Kerio Valley katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.


Rais alikuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi walioandamana naye katika ziara yake ya bonde la Ufa iliyong’oa nanga hiyo Alhamisi alipomtania mbunge wa Kapsereti Oscar Sudi kuhusu kutambulishwa kwake kama ‘mhandisi’.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Baada ya kuwatambulisha viongozi wengine wengi, Ruto alionekana kumsahau Oscar Sudi ambaye ilibidi watu kupiga kelele kumjulisha rais uwepo wa mbunge huyo mkwasi.


“Ooh, tuko na huyu injinia. Sijui ni injinia wa nini lakini tu ni injinia tusema, anaitwa Oscar Sudi. Nasikia zamani alikuwa area huku sasa amepelea uinjinia mpaka umefika Eldoret. Ahsante sana,” Ruto alisema akimtambulisha Sudi kwa umma kwa njia ya utani.


Kitembo cha Sudi katika Nyanja ya masomo kimekuwa ni mjadala pevu kwa miaka mingi sasa humu nchini.


Mbunge huyo ambaye ni mtetezi mkali wa sera za rais William Ruto alijipata kuwa gumzo la mitandaoni mwaka jana baada ya kufichua kuzawadiwa shahada na chuo kimoja.


Sudi alifichua kwamba alivishwa joho na shahada ya uzamili ya kiheshima na chuo cha Northeastern Christian wakati alipoudhuria hafla ya kufuzu kwa mahafali katika chuo anuwai cha Eldoret.


Shahada hiyo ilivutia joto la kisiasi kutoka kwa baadhi ya watu, hadi ikapelekea mamlaka inayosimamia elimu ya juu CUE kuingilia kati na kutaka shahada hiyo kuchunguzwa na kufutiliwa mbali ikiwezekana.