Waziri wa zamani wa ICT, Margaret Ndung’u ameripotiwa kukataa uteuzi wake na rais Ruto kama balozi wa Kenya kwenda nchini Ghana, wiki chache baada ya kuondolewa kwenye baraza la mawaziri.
Ndung’u alitakiwa kufika leo mbele ya kamati ya bunge kupigwa msasa kuhusu uteuzi huo mpya lakini ametoa barua saa chache kabla, akisema hatoweza kufika bungeni kwa kile alichokitaja kuwa ni sababu binafsi.
Alipaswa kufika mbele ya Kamati inayoongozwa na Mbunge wa Ubelgiji Nelson Koech ambayo inaendesha vikao vya kuidhinisha wateule hao.
Koech alisema inasikitisha kwamba kwa mara ya pili, mteule amekataa kazi ya Ghana, baada ya Vincent Mogaka kukataa uteuzi wa kwenda Ghana mwaka jana Aprili.
"Napenda kuwajulisha kuwa sitajitokeza kwa sababu za kibinafsi na za msingi," Ndung’u aliiandikia Kamati hiyo kupitia kwa Katibu wa Bunge.
"Ili kuokoa muda muhimu wa kamati, barua hii inatumika kama notisi kwamba sitahudhuria."
Hii ni mara ya pili kwa mteule kukataa uteuzi kwenda Ghana.
Mwaka jana, aliyekuwa Mbunge wa Mugirango Magharibi Vincent Mogaka Kemosi alikataa uteuzi wake kama Mwakilishi Mkuu wa nchi hiyo mjini Accra, Ghana.
Nyambura ambaye aliondolewa kwenye baraza la mawaziri kufuatia maandamano yaliyoongozwa na vijana kote nchini aliteuliwa mnamo Desemba 24, 2024, kuwakilisha nchi nchini Ghana.
Alihudumu katika wizara ya ICT kwa miezi minne kati ya Agosti na Desemba 2024 kabla ya rais Ruto kufanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri na kumteua William Kabogo kuchukua nafasi yake.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!