KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Januari 8.  

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

 

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja unusu  jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni Nakuru, Nandi, na Kisii.

Katika kaunti ya Nakuru, sehemu za maeneo ya Molo na Olenguruon zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Maeneo ya Kabiyet, Kapchumo, na Kamasia katika kaunti ya Nandi yataathirika kati ya saa mbili na robo asubuhi na saa kumi na moja unusu jioni.

Sehemu za maeneo ya Emenwa, Igare na Kigamere katika kaunti ya Kisii pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.